The House of Favourite Newspapers

Sudan: Jeshi Lagoma Kukabidhi Utawala kwa Raia, Wananchi Waandamana

OFISA wa ngazi ya juu wa Baraza la Kieshi nchini Sudan, Luteni Jenerali Salah Abdelkhalek,  amesema jeshi hilo halitaruhusu raia kuchukua nafasi za juu za uongozi katika Baraza la Uongozi nchini humo wakati wa serikali la mpito lakini watazingatia kuwapa nafasi sawa za ujumbe katika baraza hilo.

 

Baada ya kauli hiyo, waandamanaji wameendelea kuandamana kwa kukaa kwa wingi nje ya ofisi kuu ya jeshi la nchi hiyo wakitaka kuachia liachie madaraka baada kumuondoa aliyekuwa rais Omar al-Bashir, aliyeng’olea madarakani Aprili 1, baada ya kutawala Sudan kwa miaka 30.

 

Bashir aliondolewa madarakani na Baraza la Mpito la Kieshi ambalo limechukua utawala kwa raia kwa kipindi cha miaka miwili, jambo ambalo linapingwa na waandamanaji ambapo viongozi wa waandamanaji wamelishutumu jeshi kukataa kufanya majadiliano.

Viongozi wa jeshi wanasema wanahitajika kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa wanaongoza nkwausalama wa taifa hilo.

 

Wajumbe saba wa baraza  linaongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, ambaye aliliiambia shirika la utangazji la Uingereza (BBC) mwezi uliopita kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kama watafikia makubaliano na viongozi wa kiraia.

 

Viongozi wa upinzani walisema jana wanasubiri wito wa mapendekezo yao ya kufahamu baraza jipya litakuwa na wajumbe wapi.

 

Umoja wa Afrika (AU) uliupa uongozi wa kijeshi  siku 60 kulimaliza suala hilo.

Mwonekano wa makao makuu ya jeshi la Sudan.

Picha iliyopigwa na satelaiti ikionyesha makao makuu ya jeshi jijini Khartoum, eneo ambalo waandamanaji walikusanyika na kubaini kuwa limetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuanza kazi ya utawala nchini humo.

 

Kiongozi wa zamani wa Sudan, Bashir mwenye umri wa miaka 75 amehamishiwa katika gereza la Kobar lililopo  Khartoum baada ya siku kadhaa tangu kukamatwa. Mwendesha mashitaka ametaka rais wa zamani kuhojiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi.

Comments are closed.