The House of Favourite Newspapers

Sugu Kortini Tena Leo, Arudishwa Rumane

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) ‘Sugu’ na Katibu wa Kanda ya Nyasa wa chama hicho, Emmanuel Masonga wamerudishwa tena mahabusu baada ya kunyimwa dhamana na Mahakama na Hakimu Mkazi, Mkoa wa Mbeya.

 

Awali, kesi hiyo ilifikishwa mahakamani Januari 16, mwaka huu na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Joseph Pande, ambaye aliiomba mahakama izuie dhamana kwa washtakiwa kutokana na sababu za kiusalama ambapo hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Utetezi, Sabina Yongo ambaye aliiomba mahakama itoe dhamana kwa wateja wake kwa kuwa wana haki hiyo kisheria.

 

Baada ya washtakiwa hao kurudishwa mahabusu, Januari 19 walifikishwa mahakamani hapo ambapo Hakimu Mkazi, Michael Mteite, alitupilia mbali ombi la Wakili Yongo la kutaka washtakiwa wapewe dhamana.

 

Sugu na Masinfa wanatuhumiwa kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais Dk. John Magufuli pamoja na katika mkitano wao mwishoni mwa mwaka jana.

Comments are closed.