The House of Favourite Newspapers

SUGU: Mimi Si DIAMOND Wala ROMA, ‘Ningempiga’ SHONZA – Video

MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘SUGU’, amelilalamikia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kuufungia wimbo wake wa #219 akidai kuwa Baraza hilo limekuwa kama Jeshi la Polisi kwani kazi yao kubwa imekuwa ni kukamata na kufungia wasanii nyimbo zao.

 

Sugu amesema hayo Bungeni jijini Dodoma leo wakati akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 na kusema kuwa yeye siyo Diamond wala ROMA ambao nyimbo zao zimefungiwa, huku akidai ‘angempia‘ Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo.

 

“Nchi hii kila Taasisi imekuwa kama polisi, maofisa wanatembea na rula kupima samaki, dagaa utapima na rula gani? Basata nayo imegeuka kama polisi, kazi yao ni kukamata na kufungia, jana wamefungia wimbo wangu wa #291 wakati hata sijautoa. Serikali itambue tumetoka mbali na hii sanaa ya muziki.

 

“Wimbo umevuja kabla sijautoa, najiandaa kwenda studio kutoa video nashangaa BASATA hawajaniita kunihoji wameshaufungia, hawajawahi kuingia hata studio, hawajui mihangaiko wala gharama za studio, wanataka kila mtu aimbe mapenzi?

 

Naibu Waziri Shonza aliibuka na kutoa taarifa kwa Sugu kuwa, kilichofanywa na BASATA ni sahihi kwani walishaagiza kwamba kabla msanii hajatoa wimbo, lazima apeleke mashairi yake BASATA jambo ambalo Sugu hakufanya, hivyo wimbo wake umefungiwa kwa sababu ametumia maneno ya uchochezi na kutokufuata sheria.

 

Sugu alijibu taarifa hiyo kwa kusema;

“Ningempiga lakini kwa hali ya dada yangu ngoja nimuache tunmsubiri mjomba, mimi siyo Diamond wala ROMA, nitaiburuza BASATA mahakamni kwa suala hili ili wajifunze jinsi ya kuendesha nchi kwa sheria na utawala bora,” amesema Sugu.

 

SUGU: “Mimi Siyo DIAMOND Wala ROMA, Ningempiga Shonza

Comments are closed.