The House of Favourite Newspapers

Sukari yagota Sh. 3,000 bei ya chini

0

Sukari-001

Na Gabriel Ng’osha, UWAZI

Dar es Salaam: Machi 8, 2016 Serikali kupitia Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, ilitangaza  kuwa bei ya rejareja ya sukari itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja lakini mitaani bei si hiyo iliyoelekezwa ingawa bei hizo zinatofautiana eneo moja na jingine huku bei ya kawaida kwa Jiji la Dar ni shilingi 3000 kwa kilo.

Lakini suala la bei elekezi bado limekuwa ni tatizo kwa wananchi na wafanyabiashara.

Gazeti la Uwazi lilifanya jitihada za kuzungumza na wahanga wa janga la sukari wa mikoa mbalimbali ya nchini na kupata maoni yako kama ifuatavyo:

Wakazi wa Dar Omary mkazi wa Tabata kwa upande wake alisema sukari mtaani kwao ipo ila bei ndiyo iko juu, huwezi kupata kama hauna Sh. 2,800 kwa kilo moja, Fatuma wa Magomeni yeye alidai amenunua kwa Sh. 2,800 kwa kilo moja.Huku Shuu wa Mbagala akishangazwa na bei kutofautiana kila siku na kila eneo kwani kwingine ni Sh. 2, 200, 2,400 hadi 2,600.

Gasper wa Mwanza

Kwa eneo langu la Misheni hapa Mwanza kilo ni Sh. 3,000 huku Ester wa Nyegezi, alisema eneo hilo ni Sh.3,000 kwa kilo.

Habiba wa Moshi

Yeye alisema mtaani kwao sukari ni Sh. 3,000 kwa kilo na haiuzwi zaidi ya nusu. Juliana ambaye ni mkazi wa Songea alisema ananunua kwa Sh. 3,000, Godfrey wa Misugusugu, Pwani kwao kilo ni Sh. 2,700 na Omary kutoka Kondoa Mjini eneo la Тaneѕco alisema bei ni Sh. 3,600.

Sylivia wa Arusha

Kwa maeneo baadhi ya Arusha bei zinatofautiana, mtaani kwangu kilo ni Sh. 2,400 na unapewa kilo moja tu. Naye Sara aliyeko Arusha pia anadai eneo lake ni Sh. 2,500 kwa kilo na haipatikani kwenye maduka mengi.

Jacqueline wa Mbeya

Maduka mengi yameacha kuuza sukari ila bei ni 2,800 kwa kilo. Sophia wa Tunduma alisema sukari kwa eneo lake siyo tatizo, maduka yote inapatikana ila bei ndiyo 2,500 kwa kilo.

Adelina wa Zanzibar

Kwa upande wa Zanzibar sukari ni Sh. 1,500 huku Paulina mkazi wa Boma Moshi ni amesema inauzwa Sh.3,200 kwa kilo.

Gazeti la Uwazi lilifanya jitihada za kumtafuta Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwaijage lakini simu yake haikupatikana. Hata hivyo, Jumamosi iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (pichani) alifafanua kuhusu jambo hilo sambamba na kuwahakikishia Watanzania kuwa serikali imeendelea na jitihada za kuondoa tatizo hilo.

“Zipo jitihada nyingi za serikali kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini,  ambapo serikali imesambaza jumla ya tani 20,000 huku tani 35,000 zinatarajiwa kusambazwa nchi nzima, aidha naomba wafanyabiashara wasiuze sukari zaidi ya Sh. 2,200 kwa kilo,” alisema waziri mkuu.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply