The House of Favourite Newspapers

Suluhisho Bunifu za Tabianchi Zatangazwa StartUp Nne Zashinda

StartUps nne zilizochaguliwa na kupokea Euro 10,000 kwa kila moja kwa kuendeleza suluhisho za kukabiliana ya mabadiliko ya tabia nchi, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania – 3 Aprili 2025 – Climate-KIC, kwa kushirikiana na SmartLab, inayo furaha kutangaza washindi wa Programu ya Adaptation & Resilience ClimAccelerator 2025.

Baada ya Demo Day yenye mafanikio, Rada 360, Mbegu Nzuri Biotech Farms, InsectUp, na HERVEG.05 wamechaguliwa kwa suluhisho zao bunifu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wakishughulikia changamoto muhimu kama vile hatari za mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima, ukosefu wa mbegu zenye ustahimilivu wa hali ya hewa, usimamizi duni wa taka za kikaboni, na utapiamlo katika jamii za vijijini.

Mpango wa Adaptation & Resilience ClimAccelerator uliwawezesha wajasiriamali 10 waliokuwa wakibuni suluhisho za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali. Washiriki walipokea mafunzo maalum, ushauri wa kitaalamu, na fursa za kukutanishwa na wawekezaji ili kuimarisha ubunifu wao katika kukabiliana na changamoto za tabianchi.

Sehemu muhimu ya mpango huu ilikuwa Mchakato wa Tathmini na Uthibitishaji wa Ubunifu wa Adaptation & Resilience, uliotengenezwa na Climate- KIC.

Mfumo huu unawawezesha waanzishaji kupima, kuthibitisha, na kuwasilisha athari za suluhisho zao kwa wawekezaji. Kupitia tathmini za kitaalamu na uthibitishaji wa athari, wanapata sifa zinazowafanya kuwa tayari kwa uwekezaji na nafasi nzuri sokoni.

Tarehe 3 Aprili, mpango huu ulifikia hatua muhimu kupitia Demo Day iliyoandaliwa katika Hyatt Regency, Dar es Salaam, ambapo washiriki waliwasilisha suluhisho zao mbele ya jopo la majaji. Baada ya maonyesho ye nye ushindani mkubwa, waanzishaji wanne waliibuka washindi, wakichukua hatua muhimu kuelekeakupanua suluhisho zao kwa jamii zilizo hatarini zaidi nchini Tanzania.

Washindi hawa watapokea €10,000, pamoja na ushauri endelevu na rasilimali za kuharakisha ukuaji wao. Hatua inayofuata ni majaribio ya suluhisho katika jamii za vijijini, ili kuhakikisha yanafaa kwa changamoto halisi zinazowakabili watu walio hatarini zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Sophie White, Meneja Mwandamizi wa Programu, Ubunifu na Masoko Yanayoibukia – Climate-KIC, alisema:

Kupitia Adaptation & Resilience ClimAccelerator, tunatoa maarifa na nyenzo kwa waanzishaji kupima athari za suluhisho zao na kuzifanyia majaribio katika mazingira halisi. Kwa kuhusisha moja kwa moja jamii na kupitia tathmini za kina, waanzishaji hawa wanapata sifa zinazoeleweka kwa wawekezaji na wateja.

Tumeshuhudia ukuaji mkubwa wa suluhisho hizi, na tunaamini zinaweza kuleta mabadiliko halisi.

Laurian Mafuru, Mratibu wa Programu – SmartLab, aliongeza:

“Tunatarajia kuona suluhisho hizi ikijaribiwa katika mazingira halisi, zikionyesha uwezo wake wa kuenea na kuwa na ufanisi zaidi. Hatua hii ni muhimu ili kuboresha ubunifu wao na kuhakikisha unaleta

mabadiliko endelevu katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Waanzishaji hawa wanathibitisha kuwa suluhisho za mabadiliko ya tabianchi haziishii tu katika maendeleo ya kiuchumi, bali pia zinasaidia jamii za Tanzania kukabiliana na athari zake. Kwa kushughulikia changamoto kama upatikanaji wa maji, usalama wa chakula, na uharibifu wa mazingira, wanajenga uimara mahali panapohitajika zaidi.