SULUHUSHO LA UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME-2

Wiki iliyopita niliianza mada hii ambayo inaonekana kugusa wengi juu ya tatizo la upungufu wa nguvu za kieme. SASA ENDELEA… TATIZO la upungufu wa nguvu za kiume na kutofurahia tendo ni tatizo la muda mrefu na sugu ambalo uhusisha ubongo, homoni na hali ya kisaikolojia ya mtu, mishipa ya fahamu, misuli ya mwili na mishipa ya damu.

Kwa hiyo shida kubwa mno inaweza kuanzia hapa. Msongo wa mawazo na matatizo ya akili yanaweza kusababisha tatizo hili likawa baya zaidi. Wakati mwingine matatizo ya kimwili na kiakili huwa ni chanzo kikubwa katika tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume. Hofu katika uhusiano au hofu juu yako mwenyewe kwamba utadhurika au kuumia utakaposhiriki au huweza kukufanya uishiwe au upungukiwe na nguvu za kiume.

Magonjwa au matatizo yote ya kiafya huweza kuathiri nguvu za kiume mfano magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo, magonjwa ya mishipa ya damu, uwepo wa cholesterol au lehemu nyingi kwenye damu, shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari, unene wa kupita kiasi, magonjwa ya mifumo, matumizi ya sigara, magonjwa ya uume, ulevi, kulala sana au kukosa usingizi, matibabu ya saratani ya tezi dume au uvimbe wa tezi

dume, kuumwa au upasuaji wa maeneo ya nyonga. Matatizo ya kisaikolojia yanayoathiri nguvu za kiume ni kama vile magonjwa ya akili yanayoambatana na kuchanganyikiwa au kupoteza kumbukumbu, hofu ya mara kwa mara, sonona, msongo wa mawazo au ‘stress’ na matatizo katika uhusiano wa kimapenzi au uhusiano wako na watu wengine kama ndugu, jamaa na marafiki. Ila wapo watu ambao wana hatari ya kuja kupata tatizo hili siku za usoni, nao ni wale ambao wana magonjwa hasa kisukari na magonjwa ya moyo, wavutaji wa sigara, wenye unene mkubwa, wagonjwa

hasa wa saratani na shinikizo la juu la damu, watu wenye matatizo ya kisaikolojia kutokana na kukosa ajira, uhusiano wa kimapenzi na magonjwa, wanaotumia pombe kupindukia na madawa ya kulevya.

MADHARA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Kutokufurahia maisha ya ndoa au uhusiano, kuwa na msongo wa mawazo na hofu za mara kwa mara, hasa linapokuja suala la mapenzi, daima unakuwa katika hali ya kutojiamini na kushindwa kuvumilia kukaa na wanaume wenzio, daima unakuwa ni mtu wa kujitenga, kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi kwa kukimbiwa na wanawake. Pia unashindwa kumpa ujazito mkeo.

SULUHISHO

Kama huna tatizo hili, basi chagua maisha bora kwa kuepuka vyanzo tulivyoeleza. Fanya mazoezi ya mwili na hakikisha unakula chakula bora. Kama tayari una magonjwa muone daktari wako. Fanya uchunguzi wako endapo una dalili za upungufu wa nguvu hasa kama umri wako ni kuanzia miaka arobaini. Tiba itatolewa endapo una tatizo tayari kwa kuzingatia vipimo. Zipo dawa za homoni, dawa za kuongeza nguvu za kiume na dawa za kuamsha msukumo wa damu katika misuli ya uume. Dawa za homoni na za kuongeza nguvu kutolewa wakati maalum baada ya uchunguzi wa kina wa daktari.

KUAMSHA MSUKUMO WA DAMU KATIKA MISULI YA UUME

Hii ni dawa ipo kama mafuta hutumika kupaka katika uume wote na kuusugua taratibu ‘massage’. Dawa hii ina vichocheo vya kiume au testosterone husaidia kufungua mishipa ya damu ya uume, haina kemikali na inaweza kutumika na mtu yeyote kuanzia umri wa miaka 35 na kuendelea hata kama hana tatizo hili.


Loading...

Toa comment