The House of Favourite Newspapers

Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu Chadema

0

frederick-sumaye Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa, Freeman Mbowe amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

sumaye

Amesema, dhamira ya CHADEMA ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

Leave A Reply