The House of Favourite Newspapers

Utingo Malori ya Dangote Auawa kwa Kupigwa na Sungusungu – Video

0

 

Utingo wa malori ya Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Imani Abdallah Mnyoge mwenye umri wa miaka 31, mkazi wa Goroka, Kongowe jijini Dar es Salaam, ameuawa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kupigwa na sungusungu, tukio lililotokea Oktoba 16, mwaka huu.

 

Global TV imefunga safari mpaka Kongowe na kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, ambao wameeleza kwa uchungu jinsi maisha ya ndugu yao yalivyokatishwa kikatili, kutokana na kipigo cha sungusungu ambao jukumu lao la msingi ni kuwalinda wakazi wa eneo hilo na mali zao.

 

Najma Abdallah, ambaye ni mjane wa marehemu na ameeleza kwa uchungu kuhusu tukio hilo ambalo ni pigo na simanzi kwake.

 

 

Wakizungumza na waandishi wetu Richard Bukos na Issa Mnally, ndugu na majirani wa marehemu, wametoa kilio chao wakieleza kwamba, hili si tukio la kwanza kwa sungusungu wa eneo hilo, kufanya matukio ya kikatili kama hayo.

 

Global TV imemtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro na kumuuliza kuhusu tukio hilo na hatua ambazo jeshi la polisi limezichukua hadi sasa.

 

 

Leave A Reply