The House of Favourite Newspapers

Suprise: Wema Sepetu Alivyompandisha Diamond Plutnumz Jukwani – Video

Wema Sepetu mikononi mwa Diamond.

SURPRISE ya nguvu imefanyika usiku wa kuamkia leo pale Hyatt Regency Hotel baada ya Malkia wa Bongo Movies, Wema Seetu kumpandisha mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ukumbuni kwa ajili ya ufanya makamuzi.

 

Tukio hilo limetokea wakati wa hafla ya kumtambulisha msanii mpya wa Lebo ya WCB Wasafi, Mbosso ambaye amejiunga na lebo hiyo baada ya kundi lake la awali la Yamoto band kuvunjika.

 

Wema kwenye hafla hiyo.

Wakati sherehe ikiendelea, Rayvanny alikuwa akikamua, wakati akimalizia shoo alimuita Wema Sepetu ambaye aliibuka jukwaani kisha zikaanza kusikika kelele za mashabiki wakiimba …Wema…. Wema….Wema… ambaye baada tu ya kupanda na kuwasabahi mashabiki alimuita mpenzi wake wa zamani, Diamond Platinumz naye apande jukwaani.

 

Kelele ziliongezeka …Diamond… Diamond… Diamond…., haikuchukua muda Diamond akaibuka jukwaani na kukumbatiana na Wema kwa sekunde takribani 20 kabla ya kuanza kukamua.

Wakati Mond akikamua jukwaani wa wasanii wengine wa WCB, Wema alikuwa akikata mauno jukwaani hapo jambo ambalo liliamsha msisimuko na shangwe miongoni mwa mwashabiki na kelele nyingi za kuwashangilia zikitawala.

Ikumbukwe kuwa Wema na Diamond waliwahi kuwa wapenzi miaka kadhaa iliyoita kabla ya kuachana na kila mtu kuingia kwenye mahusiano mengine.

SHUHUDIA TUKIO ZIMA

Comments are closed.