The House of Favourite Newspapers

‘Suprise’ ya Harmonize Kwenye Shoo ya Rayvanny Usipime! (Picha +Video)

Harmonize akipiga shoo na Rayvanny Dar Live Mbagala, Dar, usiku wa kuamkia leo.

WAPENDA burudani wengi walijua ni ngumu mida ya saa tisa usiku msanii mwingine kutoka WCB Wasafi kuonekana katika jukwaa la Dar Live Mbagala ambako Rayvanny alifanya shoo yake aliyoipa jina la Vanny Day.

Rayvanny aliwapa ‘suprise’ mashabiki wake waliofurika kiwanjani hapo kwa kumpandisha Harmonize kwenye steji, kitendo ambacho kilifumua shangwe upya na kufanya kizizime kwa shangwe.

Harmonize alipanda na ngoma ya Paranawe ambayo ameimba na Rayvanny, ngoma hiyo iliwalipua mashabiki wengi waliokuwa wamekaa pembeni wakipata moja baridi moja moto.  Baada ya Paranawe akaja na wimbo wake wa ‘Never Give Up’ ambao kwa sasa ndiyo habari ya mjini.

Hadi anashuka stejini hakuna shabiki ambaye alipenda kitendo hicho, kwa kuwa kila mmoja alikuwa na kiu ya kumsikia Harmonize akiimba tena na tena hadi jua linatua.

Comments are closed.