The House of Favourite Newspapers

Supu ya Kichwa cha Samaki

0

LEO tutaongelea jinsi ya kupika supu ya kichwa cha samaki, inaweza kuwa aina yoyote ile ya samaki. Kuna wasiopenda kichwa lakini supu nzuri sasa niwaeleze inatoka kwenye kichwa. Basi nikwambie tu katika kichwa cha samaki kuna supu nzuri na inafaa kwa afya yako unaweza kumpatia hata mtoto.

SUPU KWA WATU 2

Nasema kwa watu wawili kwa sababu kwenye familia kama hukula na baba wewe mama utakula na mtoto kwani ni nzuri kwa lika zote.

MAHITAJI

Vichwa 2 vya samaki, maji ya limao 1, pilipili hoho 1 (Pasua kati kati ondoa mbegu na uikatekate)

Karoti 2

(zikatekate)

Chumvi kiasi utumiacho

Pilipili manga nusu kijiko cha chai

Mchanganyiko wa viungo vya mimea (mixed herbs) kijiko 1 cha chai.

JINSI YA KUIPIKA

Kwanza andaa vichwa vya samaki kwa kuvisafisha vizuri, kama upenda unaweza kuondoa macho.

Kisha weka katika chombo na uanze kuvichemsha. Weka maji, chumvi kiasi, pilipili manga, mixed herbs na uache vichemke kwa dakika 8 – 10 ndipo uweke karoti, pilipili hoho, maji ya limao kisha acha vichemke dakika chache huku ukiangalia kama vimeiva.

Ni hivyo tu supu inakuwa ipo tayari kwa kuliwa. Hapo nimeweka vitu vichache ila unaweza ongeza vingine zaidi kama kabichi au mboga zingine za majani nk.

Roma, Mziwanda, Gigy Money, Linex,Kwenye Stage Kilinuka

Leave A Reply