SURA 3 ZA ‘MISAMBWANDA’ YA MASTAA WA KIKE BONGO!

Jane Ramoy ‘Sanchi’.

SIKU moja alifika staa mmoja wa kike katika ofisi zetu kwa lengo la kufanyiwa mahojiano. Ni staa mkubwa tu wa filamu ambaye naomba kwa leo nilihifadhi jina lake. Alipofika mapokezi, akaomba kuonana na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa. Nikatoka na kumkuta ni msanii huyo ambaye nilimuomba aje kufuatia shepu yake kuwa gumzo sana mitandaoni.  Nikamchukua na kumpeleka kwenye chumba cha mahojiano. Wakati tukielekea kwenye chumba hicho, nilimuacha yeye atangulie, kwa nini? Kwa sababu nilitaka kuthibitisha kile ambacho nimekuwa nikikiona kwenye mitandao, kwamba yaliyomo yamo?

Nilichokiona kilinistaajabisha sana. Hakuwa na cha kalio chochote, sehemu yake ya nyuma ilikuwa flati kabisa. Hapo ndipo nilipogundua kuwa, hawa mastaa huwa wanatufanyia kamchezo wanapoposti picha zao kwenye mitandao.

Haikuishia hapo, wakati tukiwa kwenye mahojiano, nikamuuliza swali la kizushi kwamba, mara kadhaa anapoposti picha zake kwenye mitandao zikionesha amefungashia watu wamekuwa wakimkebehi kwamba anatumia dawa za Kichina, nikamtaka aniambie ukweli huku nikiwa nimemkazia macho.

Kiukweli alionesha uso uliotahayari. Ni kama mtu aliyesema kimoyomoyo; NIMEUMBUKA! Na kweli alikuwa kaumbuka kwa kuwa, kiuhalisia hakuwa na msambwanda kama ambavyo amekuwa akijinadi. Na hapo ndipo alipoamua kuniambia ukweli. Sikia alichoniambia;

“Labda nikuambie tu ukweli wa kilichotokea kwenye shepu yangu lakini naomba usiandike. Ni kwamba, miaka ya nyuma kidogo kuna dawa niliambiwa ukiipaka, kalio linafutuka. Mimi nilikuwa na ulimbukeni wa kutaka kuwa na kalio kubwa hivyo nikainunua dawa hiyo na kuitumia.

“Baada ya siku kadhaa, nikaanza kuona mabadiliko. Shepu ikawa shepu kweli lakini kuna wakati nikaacha kutumia ile dawa. Hapo ndipo nilipoanza kuona madhara yake. Nilitokwa na madonda ambayo sikuyaelewa. Nikawa nawashwa sana! Hali hiyo ilinifanya niende hospitali ambapo kuna daktari mmoja pale Muhimbili alinisaidia sana, nikapona lakini ‘mzigo’ wote ukawa umepotea.

“Sasa nikawa naona aibu kuvaa nguo za kuonesha shepu, nguo zangu zikawa ni madera. Ikiwa kuna sehemu nataka kwenda ambako n’tatakiwa kuvaa suruali au gauni ambalo litaonesha shepu, nilikuwa navaa taiti flani ambazo zimetengenezwa maalum kabisa zikiwa na kalio. Kwa hiyo ukivaa kisha ukavaa na suruali au gauni la kubana, atakayekuona atajua umefungashia kumbe hamna lolote.”

Simulizi ya staa huyu imenifungua kwenye suala la hizi shepu za mastaa wetu wa Bongo. Kumbe wanaume wala hawatakiwi kuchanganyikiwa wanapoona mastaa hawa wametupia picha zinazowaonesha wana makalio makubwa. Baadhi yao hawana lolote, ni mbwembwe tu za kwenye mitandao lakini ukikutana nao laivu utastaajabu.

Kwa wasiojua basi ni vyema wakajua leo kwamba, shepu za mastaa wa kike Bongo ziko katika sura tatu. Wapo mastaa ambao kweli wamejaaliwa shepu matata. Kwa mfano mwanadada Jane Ramoy ‘Sanchi’. Huyu wakati anaanza kuonekana wapo waliomtuhumu kwamba naye anaweka vigodoro. Ikafika wakati akajitoa ufahamu na kupiga picha za utupu kabisa. Hapo ndipo watu walipoamini kwamba, kalio lake ni ‘OG’.

Kutokana na uhalisia huo, baadhi ya watu wakaanza kuvumisha kuwa anatumia dawa za Kichina maana huko nyuma hakuwa hivyo. Napo akaona awakate vilimilimi washakunaku, akatupia picha akiwa amesimama na mama yake. Kumbe mama yake naye ‘mashalaa’ ana bonge la shepu na ndipo ikathibitika kuwa, kalio lake ni halisi na ni la kurithi kutoka kwa mama yake.

Kwa hiyo kuna mastaa sampuli ya Sanchi ambao kweli misambwanda yao ni orijino. Lakini kuna mastaa wengine ambao makalio yao yametokana na kutumia dawa za Kichina. Hawa inaweza kuwa ngumu kuwataja kwa kuwa ushahidi unakosekana ila wapo ambao kipindi cha nyuma walikuwa na makalio makubwa na sasa yamesinyaa. Hawa ndiyo wale wa kutumia dawa za kuongeza makalio.

Lakini sasa, asilimia kubwa ya mastaa Bongo wanatumia staili ya kuweka vigodoro ili kutengeneza shepu. Wanavaa zile taiti ambazo zenyewe zina kalio tayari, sasa ukijumlisha na vile kikalio vyao, unashangaa shepu hiyooo, kumbe ni feki.

Wengi wao wamekuwa wakiumbuka maana taiti hizo si za kuvaliwa kila mahali. Ndiyo maana wapo ambao wamekuwa wakiumbuka wakiwa beach ambako huwezi kuvaa nguo za kuogelea na taiti ya kalio. Sehemu nyingine ambako mastaa hawa wanaumbuka ni pale wanapokuwa faragha na wapenzi wao kwa mara ya kwanza. Utashangaa wakati unamuona klabu alikuwa na kalio kubwa lakini amevua nguo kikalio kama cha mtoto.

Ushauri wangu ni kwamba, ni vyema mastaa wakajikubali vile Mungu alivyowaumba. Kama huna kalio, huna tu! Hii kutafuta makalio feki ni kujisumbua tu ambako mwishowe utaumbuka!

Makala: Amran Kaima, Uwazi

Loading...

Toa comment