The House of Favourite Newspapers

Suzy Asherehekea Birthday Kimaajabu (Picha +Video)

 MTANGAZAJI wa kituo cha EATV, Suzane Benard ‘Suzy’ jana asubuhi amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kimaajabu ambapo amejichanganya na wakina mama wanaofagia barabarani na yeye kufagia.

Mtangazaji wa kituo cha EATV, Suzane Benard ‘Suzy’ (kulia) akifanya usafi na barabara ya Shekilango kisha akapita Sinza-Madukani na kumalizia Sinza-Mori.

 

Ishu nzima ilianzia barabara ya Shekilango kisha akapita Sinza-Madukani na kumalizia Sinza-Mori ambapo alijichanganya na watu wa usafi kufagia nao mwanzo mwisho.

 

Katika kujichanganya huko, Suzy alipata pia nafasi ya kuwauliza mawili-matatu ambapo walikiri kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo vifaa vya usafi pamoja na vikinga pua.

Suzane Benard ‘Suzy’ akiendelea kufanya usafi.

Hata hivyo, Suzy hakuwaacha hivyohivyo kinamama hao, aliwapa mafagio, vikinga pua pamoja na vifaa vingine vya barabarani na mwisho akatoka nao hadi kwa Shilole (Shishi Trump) kupata nao chakula cha mchana.

Comments are closed.