The House of Favourite Newspapers

Suzy kutoa sapraiz kwa wafanya usafi barabarani

SUZANE Benard ‘Suzy’ ambaye ni mtangazaji wa EATV leo (Jumamosi) anatarajia kutoa sapraiz kwa wanawake wanaofanya usafi barabarani ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Suzy alisema mastaa wengi wamekuwa wakisherehekea siku zao za kuzaliwa kwa kuwaangalia watu wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wagonjwa lakini kwake ameamua kuja kivingine kwa kujichanganya na wanawake wanaohatarisha maisha yao katika kufanya kazi ya usafi barabarani.

 

“Nikiwa kama mwanamke, nawaona wanawake wenzangu wakifanya usafi huu katika wakati mgumu, kuna wengine wanaishia kujifunika na nguo tu puani kwa hiyo kesho (leo) nitahakikisha naingia na mimi barabarani kushiriki nao usafi, baada ya hapo nitawaachia sapraiz ambayo wataiku mbuka maishani mwao,” alisema Suzy.

 

Stori: Mikito Nusunusu

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.