The House of Favourite Newspapers

SUZY: Kwapa Limenipa Madili

BAADA ya kuandamwa mitandaoni kuwa anakera kwa kufuga nywele za kwapani na kuzianika, mtangazaji Suzan Benard ‘Suzy’ amefunguka kuwa kwapa limempa madili.

 

Akichonga na Za Motomoto, Suzy alisema anawashangaa waliokuwa wakimnanga mitandaoni bila kujua kwamba ana malengo yake ambayo yameanza kutimia.

 

“Nimepata madili mengi tu mojawapo ni la mafuta ya kujipaka mwilini (anataja jina), sasa waendelee kuchonga mwenzao nitaendelea kuzifuga na kuzitunza zaidi ya hapa,” alisema Suzy.

SUZY “Mwanaume Wangu Anapenda Nywele za Kwapa” – BEAUTY & STYLES

Comments are closed.