The House of Favourite Newspapers

Sven Afichua Jambo la Luis

0

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa ilikuwa lazima kumuweka benchi winga wa timu hiyo, Luis Miquissone katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ili kuwa na uhakika wa kumpata mchezaji huyo katika mchezo unaofuata wa ligi dhidi ya Yanga.

 

Miquissone katika mchezo huo, hakuwa katika kikosi cha Simba kutokana na kuhofia kupewa kadi ya njano ya tatu, jambo ambalo lingemfanya kukosa mechi inayofuata kwani katika michezo miwili iliyopita, winga huyo alipewa kadi mbili za njano – moja katika kila mechi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha huyo alisema kuwa waliamua kumpumzisha winga huyo ili kuwa na uhakika wa kumpata katika mchezo dhidi ya Yanga, kwani kama wangemchezesha lolote lingeweza kutokea.

 

“Kumchezesha Luis akiwa na kadi mbili katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ni kama kubahatisha kumpata katika mchezo wetu unaofuata dhidi Yanga, kwa upande wetu tuliona ni sahihi kutocheza kabisa ili tuwe na uhakika naye.

 

“Benchi la ufundi tulikuwa tunafahamu juu ya suala hili na hata kwake Luis alikuwa anafahamu juu ya hili, hivyo hata kama tungempa nafasi ya kucheza, naamini angecheza huku anawaza kuhusu kupata kadi na hiyo si sawa kwani tunahitaji mchango wake kwa asilimia zote,” alisema kocha huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

 

Leave A Reply