Sven Awajibu Mashabiki Simba SC

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amewajibu mashabiki wa Simba kuhusu jina lake la utani ‘kishingo’.
Alipojiunga na Simba mashabiki wa timu hiyo walimpa jina la utani ‘kishingo’ kutokana na muonekano wake.Sven ambaye alikinoa kikosi cha Simba kwa mafanikio makubwa akiifi kisha timu hiyo kwenye Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sven aliacha kukinoa kikosi hicho mwanzoni mwa msimu huu na kutimkia nchini Morocco ambapo kwa sasa anainoa timu ya Far Rabat inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Tangu aanze kukinoa kikosi hicho Sven hajapoteza mchezo wowote na kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya nne kwenye msimamo.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram alipojibu swali la shabiki yake ambaye aliandika kuwa: “Alikuwa akifahamu kuwa mashabiki walimpachika jina la Kishingo?Sven alijibu kuwa “Ni bora uwe na shingo ndefu kuliko kuwa na kichwa kikubwa.
STORI: LEEN ESSAU,Dar es Salaam

