The House of Favourite Newspapers

Swahiba wa Lowassa Ataitiwa Harusini kwa Prof. Jay

0
Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Rwakatare akimshikilia Hamisi Mgeja wakati wa taharuki hiyo.

 

MWENYEKITI wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja ambaye ni swahiba mkubwa wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi Jumamosi alitaitiwa vibaya ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini hapa, Uwazi linakupa A-Z ya tukio zima.

 

KWA NINI UKUMBINI?

Mgeja alikuwa mmoja kati ya waalikwa katika sherehe ya harusi ya Mbunge wa Mikumi (Chadema) Joseph Haule anayefahamika zaidi kama Profesa Jay, ambaye alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Grace Mgonjo, mama wa mtoto wake wa kike, Lisa.

 

Katika meza aliyokuwa amekaa Mgeja, baadhi ya waalikwa wengine walikuwa ni pamoja na wabunge wa Chadema, ‘mapatna’ zao, akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, ambaye pia anatokana na Chadema, Godbless Lema.

 

James Mbatia akimsaidia Wilfred Rwakatare

 

SASA IKAWAJE?

Shughuli hiyo iliyokusanya watu wengi maarufu kwa wakati mmoja ukumbini, wakiwemo wanasiasa wa vyama vyote na wasanii wakubwa, ilikuwa ikiendelea na ratiba yake ya kawaida wakati jambo lisilo la kawaida lilipotokea katika meza aliyokaa kada huyo wa zamani wa chama tawala.

HALI YA HEWA YACHAFUKA

Wakati macho na kamera nyingi zikiwa jukwaani, ambako mmoja kati ya wasanii wakubwa alikuwa akifanya makamuzi, ghafla watu waliokuwa katika meza aliyokaa Mgeja walisimama na kuonekana wakifanya juhudi za kumtuliza kiongozi huyo, aliyekuwa amepandwa na jazba kali.

 

 

Edward Lowassa, Freeman Mbowe na James Mbatia wakishangaa varangati hilo.

 

Uwazi lilimuona Mgeja akiwa na hasira, akijaribu kuondoka mikononi mwa Lema, aliyekuwa amemtaiti kiasi cha kumfanya ashindwe kuondoka kuelekea kwa mtu anayedhaniwa kuwa alimchokonoa, akisaidiwa na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Rwakatare.

 

LOWASA, MBOWE WATAHARUKI

Waziri mkuu wa zamani Lowassa, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho, waliokuwa wamekaa meza ya pili, walipatwa na taharuki na kubaki wameduwaa, kufuatia timbwili hilo lisilotarajiwa, ambalo hata hivyo lilidumu kwa muda mfupi licha ya kuibua hofu kwa waalikwa.

Viongozi hao waligeuza vichwa vyao kutazama tukio hilo ambalo lingeweza kutia doa shughuli hiyo iliyokuwa ya kihistoria, lakini waalikwa waliokuwa pamoja naye, wakiongozwa na Lema walihakikisha haliharibiki jambo.

 

Godbless Lema akiteta jambo na Rwakatare wakati Mgeja akiwa ameketi katikati baada ya taharuki hilo.

 

ATULIZWA, AFUNGUKA

Viongozi hao walijitahidi na kufanikiwa kumtuliza Mgeja, mmoja wa viongozi waliokuwa

wakimuunga mkono Lowassa, wakati akijaribu karata yake ya kutaka kuwania urais kupitia CCM. Akiwa bado na hasira, shati lake lilionekana kuloa.

Baada ya kutulizwa, Uwazi lilimsogelea na kutaka kujua nini kilitokea na hiki ndicho alichokisema; “Mtu kama yule hawezi kuniletea dharau kama zile, wangeniachia nimnyooshe tu,” alisema bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Kashkashi hizo zilishuhudiwa pia na waziri mkuu mstaafu mwingine, ambaye kama Lowassa, naye amejiunga na Chadema, Frederick Sumaye.

 

Hali ilivyokuwa baada ya ugomvi huo kumalizika.

 

BAADAYE, KILAJI KAMA KAWA

Uwazi, ambalo lilikuwa makini kufuatilia nyendo za Mgeja baada ya tukio hilo, lilimshuhudia akiendelea ‘kukata kilaji’ kama kawaida bila kujaribu tena kuinuka hadi muda wa kurejea nyumbani ulipowadia.

 

Mgeja akipata kinywaji.

 

Sherehe hizo za harusi, zilifuatia kitendo cha kufunga ndoa kufanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, lililopo Posta ya zamani.

Baadhi ya wasanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva ambao walipata nafasi ya kuimba ikiwa kama zawadi kwa mkongwe huyo wa Bongo Fleva, ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Ambwene Yesaya ‘AY’ na mwanadada Judith Mbibo ‘Lady Jaydee.

Wosia Mzito Aliopigwa Prof. Jay na Viongozi na Wabunge wa Pande Zote

Leave A Reply