The House of Favourite Newspapers

SWAHILIFLIX Inaweza Kuwajenga au Kuwabomoa Bongo Muvi!

HIVI karibuni kampuni mpya ya kusambaza kazi za wasanii wa filamu ilianzishwa ambapo imewachukua mastaa mbalimbali wa fani hiyo ili kufanya nao kazi.

 

Habari zinaeleza kwamba kampuni hiyo ambayo itakuwa inauza na kusambaza kazi za wasanii hao kupitia mtandao inamilikiwa na Waganda ambapo wasanii ambao wamechukuliwa kwa ajili ya kufanya nao kazi hivi karibuni wameonekana kujiachia sehemu mbalimbali visiwani Zanzibar. Kama msemo usemavyo; penye wengi kuna mengi.

 

Ndiyo maana tunawaletea makala hii kama tahadhari kwenu nyie mastaa ambao mmechaguliwa kufanya kazi na kampuni hiyo ya Swahiliflix ili iwasaidie maana inaweza kuwajenga au ikawabomoa kabisa na kama hamtakuwa makini. Mara nyingi wasanii wa Bongo Muvi wamekuwa wakianzisha au kuanzishiwa vitu vingi lakini wanashindwa kuviendeleza na kuishia kufa jambo ambalo limesababisha hata soko la filamu kufa.

 

Kabla ya kuanzishwa kwa Swahiliflix kuna kampuni nyingine ilianzishwa kwa ajili ya kuuza na kusambaza
kazi za wasanii wa filamu na muziki iliyokuwa ikitambulika kwa jina la Barazani lakini haijulikani imeishia wapi kwani hakuna kinachoonekana kinaendelea mpaka sasa.

 

TAHADHARI Tahadhari ni nzuri kabla hatari haijatokea. Swahiliflix inaweza kuwa ni kampuni ambayo iko ‘siriaz’ kweli katika kufanya kazi na wasanii wa Bongo Muvi lakini wahusika ambao ni mastaa hao wakawaangusha kutokana na mambo yao wanayopenda kuyaendekeza. Wasanii wa Bongo Muvi mkitaka kampuni hii iwajenge na kurudi kuwa juu kama zamani mnatakiwa kuyaepuka yafuatayo;

 

UMBEA NA MAJUNGU Wasanii wengi Bongo Muvi mmekuwa mkiendekeza sana umbea na majungu mambo ambayo yanawarudisha nyuma kimaendeleo ya sanaa yenu maana kama sehemu mnashikana umbea kila kukicha mnakuwa mnasuluhisha ugomvi tu na muda wa kuwaza au kufanya kazi kwa ubunifu unakuwa haupo.

 

Pamoja na hilo kupigana majungu ndiyo zaidi kwani wenyewe kwa wenyewe mnasengenyana hamko kitu kimoja hivyo kama mtaweza kuepukana na haya mambo, kampuni hii inaweza kuwasaidia.

 

UBAGUZI/MAKUNDI

Ubaguzi au kuwa na makundimakundi kunadhoofisha maendeleo ya kitu chochote hivyo hata kwenu mastaa ambao mmepata nafasi ya kufanya kazi na kampuni hii mnatakiwa kuyaepuka hayo. Ni mara nyingi sana mmekuwa mkiendekeza makundi na ubaguzi jambo ambalo limekuwa ni moja ya sababu kubwa ya kuanguka
kwenu kisanaa, kumbukeni dhambi ya ubaguzi haijawahi kumwacha mtu salama maana unaweza kumbagua hata baba au mama yako, kaeni mbali na hili.

KULOGANA

mkituhumiana kulogana yaani mnashikana uchawi kama ndivyo basi mnatakiwa safari hii mbadilike na muachane na tabia hiyo. Lakini kama kweli kuna wanaowaloga wenzao wanatakiwa kuacha kwani hivyo vitu vinarudisha nyuma maendeleo ya sanaa na nyie wahusika kwa ujumla pia ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu aliyewaumba kwa mfano wake.

STAREHE

Mastaa mnaofanya kazi na kampuni hiyo ya Swahiliflix kila mmoja ameshalipwa chake ili aanze kufanya kazi, mnatakiwa kuachana na kuendekeza starehe kwani zitawatokea puani. Mastaa mmekuwa kila mnapokuwa na fedha mnajiachia sehemu mbalimbali kuponda starehe badala ya kufanya kazi nzuri na zenye ubunifu hivyo kujikuta mkitoa kazi zilezile zenye maudhui yaliyozoeleka yaani mapenzi tu.

 

Kwa sasa badilikeni kweli kama mnataka kuirudisha ile Bongo Muvi yenyewe, itumieni vizuri kampuni hii inayofanya kazi na nyie ili kuweza kufufua sanaa ya filamu upya, hii itawasaidia sana.

 

Kama kampuni hii imewaamini na kuamua kufanya kazi na nyie basi nanyi kuweni waaminifu, kuweni makini na kazi kwani ndiyo msingi wa maisha yenu na jamii pia Mara nyingi wasanii wa Bongo Muvi mnapokuwa pamoja mmekuwa inaweza

MAKALA: Mwandishi Wetu

Comments are closed.