The House of Favourite Newspapers

Sweden Mbioni Kujiunga na Umoja wa NATO Licha ya Onyo Kali Kutoka Urusi

0
Wanajeshi wa Sweden wakilinda usalama nchini humo

SWEDEN imethibitisha kuwa itawasilisha maombi ya kuwa mwanachama wa NATO katika mabadiliko makubwa ya kihistoria kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

 

Leo Jumatatu, Waziri mkuu wa Sweden Magdalena Andersson anatarajiwa kwenda bungeni kupata uungaji mkono kwa ajili ya maombi hayo, na pia ataongoza kikao maalum cha baraza la mawaziri kuzungumzia suala hilo.

Hatua hii inakuja baada ya chama chake cha Social Democratic party kuacha upinzani wake wa muda mrefu wa kujiunga na muungano wa Nato.

Jumapili Andersson alisema kutofungamana na upande wowote kwa jeshi kuliisaidia pia Sweden miaka iliyopita, lakini huenda isifanye hivyo siku zijazo.

Leave A Reply