The House of Favourite Newspapers

Szczesny: Nilimbetia Messi Euro Milioni 100 Kuwa Hapewi Penati, Siwezi Kumlipa

0
Tukio lililosababisha Argentina kupewa mkwaju wa penati

GOLIKIPA wa Timu ya Taifa ya Poland na klabu ya Juventus ya nchini Italia Wojciech Szczesny ameibuka na kusema kuwa alicheza kamari na mshambuliaji wa Argentina na klabu ya PSG Lionel Messi kuwa timu yake ya taifa isingeweza kupewa mkwaju wa penati katika tukio ambalo lilichunguzwa na VAR na baadaye kuamuliwa mkwaju wa penati ambao Messi alikosa.

 

Katika kamari hiyo Szczesny alimuahidi Messi kuwa angeweza kumpatia Euro Milioni 100 endapo kama VAR ingeamua kuwa Argentina wapewe mkwaju wa penati, na baada ya uchunguzi wa VAR iliamuliwa mkwaju wa penati upigwe, ingawa katika tukio hilo Szczesny ameoneshwa kushangazwa na namna VAR ilivyotoa maamuzi ambayo yeye binafsi anaamini hayakuwa sahihi.

Nyota wa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi alikosa mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Poland

“Hapana sikufikiria (Kuhusu kama Argentina wangeweza kupewa mkwaju wa penati). Tuliongea kabla ya penati na nikabeti ntampa Euro Milioni 100 kama Argentina watapewa penati.

“Kwahiyo nimepoteza kamari dhidi ya Messi, Sijui kama inaruhusiwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia, Yamkini naweza kufungiwa kutokana na tukio hilo, sijali.

 

Licha ya Messi kukosa mkwaju wa penati lakini Argentina ilifanikiwa kushinda jumla ya mabao 2-0 na kutinga katika hatua ya 16 bora pamoja na Poland iliyomaliza katika nafasi ya pili ya kundi hilo.

Leave A Reply