The House of Favourite Newspapers

T.B Joshua atua Dar kushuhudia kuapishwa Dk. Magufuli

0

TB JOSHUA (1)

Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa.

TB JOSHUA (3)

Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli wakibadilishana mawazo na Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua mara baada ya kuwasili nchini jioni hii.

TB JOSHUA (4)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es Salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

TB JOSHUA (2)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha na Freddy Maro)

Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.

TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt. Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

Leave A Reply