Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, aka Mnyama, leo amepata heshima ya kipekee ya kuzungumza kwenye mkutano wa RC Makonda, viongozi wa mkoa na waandishi wa habari ikiwa ni siku chache tangu atoke selo ambapo ametoa ushuhuda wa jinsi madawa ya kulevya yalivyomuathiri kwenye maisha yake.
TID ameapa mbele ya Makonda na wadau wengine kwamba hatarudia kutumia madawa ya kulevya na atakuwa mstari wa mbele kuwashauri wasanii na vijana kuachana na matumizi ya madawa kwa sababu ni hatari kwa maisha yao na ustawi wa taifa.
Hivi karibuni, TID alikuwa miongoni mwa wasanii kadhaa waliotajwa na Mheshimiwa Makonda kutumia madawa ya kulevya ambapo aliitwa Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa, baadaye akashikiliwa kwa siku mbili na wasanii wenzake kadhaa kabla ya baadaye kuachiwa mahakamani kwa masharti ya kuwataka wakabadili mienendo yao.
PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS
Comments are closed.