The House of Favourite Newspapers

T.I Amptupia Dongo Donald Trump

0

ti-donald-trump

T.I na Bw. Donald Trump

STORI kubwa kwa sasa nchini Marekani ni kuhusu vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Kama ilivyo Tanzania, hata nchi nyingine ni vivyo hivyo kwani watu huonesha hisia zao kwa kuamua kusapoti mtu flani au chama flani.

Rapa maarufu duniani T.I amekuwa ni staa mwingine kuonesha hisia zake za kumpinga tajiri mkubwa mkubwa nchini Bw. Donald Trump anayesaka tiketi ya kuwania urais kupitia Chama cha Republican.

 T.I. ameungana na mastaa wengine kibao wanaompinga Trump kuwania urais wa nchi hiyo, wamo akina Chris Brown, Mac Miller, na Frank Ocean ambao pia hivi karibuni walionekana kumpinga Trump.

Maneno ya T.I kwenye mtandao wa Instagram:

“Sawa, Je, hivi ndivyo tunavyofanya Amerika?” “Huyu ni mwakilishi tunayemhitaji aiongoze Dunia?

Hatumhitaji mbaguzi wa rangi, dini, au Chama iwe Democratic au Republican…… Taifa kubwa kama hili tusitegemee haya mambo yafanyike….. Anafanya utani na demokrasia….. Haijalishi nani utampigia kura, chama wanachokiwakilisha, au kwa nini unawachagua. Swala ni kupiga kura!!!..

tr

trm

Leave A Reply