The House of Favourite Newspapers

Taa ya gari haifungwi chumbani

WAAREEEEE miye ndiye dokta nimeachiwa hospitali wagonjwa wote ruksa kutibiwa bure, kulala bure hata wakitaka ruhusa nawaruhusu! Unaloooo bibiyeeee ulidhani ukivaa lemba ndiyo heshima wakati hata wasio wema wanalivaa! Heee heeeiyaaaa!  Wanakwambia chezea taa inayowaka kuliko kucheza gizani unaweza kushika visivyoshikika, upo nyonyo! Shoga kila siku nauona mji ulivyo mzito huu tena umejaa kila aina ya uzito! Usione unapishana na mtu anacheka ukajua alipotoka ana furaha kumbe ameacha majanga!

Shoga hakuna siku inayonipita hivihivi bila kunishika hapa! Yaani leo limenikamata kooni nikajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu! Sawa hatukatai wakati mwingine tunasema sisi wanawake mwalimu wetu kipofu lakini vingine shoga ni kama upofu tunajitakia.

Nilishawahi kuliongelea hapa suala la kutunza kucha na matumizi yake. Nikaelezea uzuri wa kucha unapokuwa na mumeo tena kwenye sita kwa sita lakini nashangaa shoga unakuwa kama umewekea taa ya kibatali kwenye ubongo, leo linapita huku kesho kule unasahau na kuanza kuuliza tena matumizi yake, weee naweeee!

Hebu weka mafiga yako mawili chini leo nikung’ate sikio shoga yangu! Siyo nakuambia kitu kesho unanitumia meseji na kuanza kulalamika mkeo hakufanyii inavyotakiwa. Jamani raha ya chumba mwanga uongo?

Kwanza chumba kikiwa na mwanga unaweza kuona kila kitu, unaweza kufurahia hata na mwandani wako mnapokuwa kwenye chakula cha usiku, au nadanganya? Hii tena ikukae akilini shoga, ni kama hesabu ukichukua mbili ukatoa moja inabaki moja, upo nyonyo?

Nimeamua kuwapa somo wale wanawake wenzangu wote ambao wao hawajui hata matumizi ya shuka, matumizi ya mishumaa chumbani hadi matumizi ya taa jaaamaaaani! Mwanamke hujui hata kutandika shuka, hujui hata kupamba meza ya vipodozi wala nguo kwenye kabati!

Achana na hayo shoga leo nimeamua kukufunda wewe ambaye hujui matumizi ya taa, wee kila mumeo akitaka kula chakula cha usiku unataka akazime taa, inahu? Unataka kila jambo ufanyie gizani atajuaje kama kuna kasoro? Mbona mambo mengine unafanyia kwenye mwanga?

Kwa taarifa yako tu shoga yangu, taa ya gari haifungwi chumbani, chumba hakitakiwi kuwa na mwanga mkali kama wa gari na ukifika ule muda wa chakula basi taa inatakiwa kubaki hivyohivyo ili mumeo ajue chakula anachokula ni chenyewe, hadi akishiba anakiona na kujiweka pembeni, upo?

Kwa leo niishie hapa nisiwe muongeaji sana mpaka mate yakanidondoka. Ni mimi Shangingi Mstaafu ukipenda waweza kuniita Anti Nasra.

Comments are closed.