TAARIFA KWA UMMA KATAZO LA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI KATIKA SAILI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu wadau wake hususani waombaji kazi kupitia Sekretarieti hiyo kuwa kuanzia mwezi Machi 2019 hakuna msailiwa atakayeruhusiwa kuingia na kifaa chochote kinachoweza kupiga picha, kunukuu maandishi nakurekodi sauti ndani ya chumba cha usailiisipokuwa kwa wale wenye mahitaji maalum.

 

Hatua hii imefikiwa kutokana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kadhaa nyakati za usaili kwa baadhi ya wasailiwa hasa saili za kuandika (written Interview) kwenda kwenda kinyume na taratibu wanazopewa ikiwemo kuzima simu na vifaa mbalimbali vya kielektroniki vinavyoweza kupiga picha nakunukuu sauti au maandishi.

 

Hata hivyo wapo baadhi ya wasailiwa wachache ambao wamekuwa wakiwasha simu ndani ya chumba cha usaili na wengine kuzitumia kutafuta majibu ya maswali ama kuwatumia watu wengine walioko nje ya chumba cha usaili kwa ajili ya kuwatafutia majibu.

 

Sambamba na hilo baadhi ya wasailiwa wamekuwa wakivitumia vifaa hivyo kupotosha umma nyakati nyingine kwa kutuma taarifa za uongo ama kuanzisha vurugu pindi wanapoona usaili umewashinda na badala yake kusingizia taratibu hazijawekwa sawa ili kuwavuruga wale waliojiandaa vizuri.

 

Kwa mantiki hiyo kila mwombaji kazi atakayeitwa kwenye usaili wa kuandikaambaye atakuja na kifaa chochote cha kielektroniki na hana mahitaji maalum anashauriwa kutafuta sehemu ya kukiachakama vile kwenye gari, au kumkabidhimtu ambaye yupo njeya chumba cha usaili, Aidhaendapo msailiwa ataingia nacho kinyume na taratibuna maelekezo hayahatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kuondolewa katika mchakato wa usaili husika.

 

Tunawashauri wasailiwa wote wanapoona majina yao ya kuitwa kwenye usaili wasome tangazo zima ili kuelewa maelekezo yote muhimu ikiwemo sehemu ya kufanyia usaili, siku na tarehe ya usaili, muda wa usaili na

namba yake ya usaili kwa kuviandika mahali ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima wakati wa usaili.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 22 Februari, 2019

Toa comment