The House of Favourite Newspapers
gunners X

Noti za Tanzania Hazitunzi Virusi vya Corona – BoT

0

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema noti zake zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti.

 

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa umma leo Alhamisi 19, 2020, imesema kwamba kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, inawashauri wananchi kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka zenye dhamana ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers), jambo ambalo  litasaidia kuua vimelea kwenye mikono.

 

“Aidha, tunawashauri wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama vile simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti.

 

“Kama ilivyotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Ugonjwa wa Corona ni tishio duniani kote na tayari umeingia nchini tangu Jumatatu Machi 16, 2020 kwa mgonjwa wa kwanza kupatikana mkoani Arusha na wagonjwa wengine wawili mmoja huko Zanzibar na mwingine jijini Dar es Salaam ambao walitangazwa jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa wa Corona (COVID-19) hapa nchini kufikia watatu.

 

“Tunawasihi wananchi katika kipindi hiki ambacho taifa liko katika mapambano dhidi ya COVID-19 kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa virusi vya Corona,” imesema taarifa hiyo.

Leave A Reply