Taarifa ya Huduma Mpya WhatsApp, Utashangaa!

 

MTANDAO wa maarufu wa Kijamii wa WhatsApp umenuia kuweka ukomo wa utumaji ujumbe kwa wanachama wake na sasa si zaidi ya mara tano, kwa lengo la kukabiliana na kuenea kwa habari za uongo kwenye jukwaa lake.

 

Wakati whatsApp wakichukua hatua hiyo, tayari mtandao mwingine wa kijamii wa Facebook tayari ulikwishaanzisha sera kama hiyo yapata miezi sita iliyopita huko nchini India.

 

Hatua hiyo inafuatia idadi kubwa ya magenge ambayo yanatumia majukwaa hayo kusambaza taarifa zisizo sahihi kwa jamii, ambapo mpaka sasa, watumiaji wa mitandao hiyo mahali kwingineko ulimwenguni, wanaweza kuchukua ujumbe na kuutuma kwa mwingine zaidi ya mara ishirini.

 

Programu hiyo ya matumizi na sheria mpya vilitangazwa katika sherehe fupi mjini Jakarta, nchini Indonesia. Inaarifiwa pia kuwa nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mwezi wa nne mwaka huu.

 

Kampuni ya Facebook ililiambia shirika la utangazaji la Uingereza  (BBC) kwamba imefanya maamuzi hayo baada ya uchunguzi makini na kupata matokeo ya uchunguzi iliyoufanya kwa muda wa nusu mwaka nchini humo.

 

Mtindo wa kutumiana ujumbe ulidhibitiwa una lengo la kupunguza jumbe za kutumiana baada ya kuupata kutoka sehemu nyingine duniani, ametaarifu msemaji wa kampuni hiyo.

 

“Hali hiyo ama umuzi huo utausaidia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kufuatilia kwa makini zaidi  jumbe binafsi na mawasiliano ya karibu. Tutaendelea kusikiliza maoni ya mtumiaji kuhusu uzoefu wake, na baada ya muda, tutaangalia njia mpya za kushughulikia maudhui na virusi, ” ilisema taarifa.

 

Kizuizi hicho kimekuja wakati WhatsApp na huduma nyingine za Facebook ziko chini ya uchunguzi kutokana na wajibu wao katika kueneza propaganda na taarifa zisizo na ukweli kwenye mitandaoni yao.

 

Wiki iliyopita, mtandao wa kijamii wa Facebook ulitangaza kuondoa kurasa mia tano pamoja na akaunti za watu wanaodaiwa kuhusika katika habari zisizo na ukweli Ulaya ya kati, Ukraine na nchi nyingine za mataifa ya Ulaya ya Mashariki .

 

Siku za karibuni pia mtandao huo ulitangaza kuanzisha kitengo kitakachotoa huduma ya kufuatilia usahihi wa taarifa na maudhui katika majukwaa yake

 

Hata hivyo, matumizi hayawekei vizingiti baina ya watu wawili kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo jumbe zake zinaweza tu kusomwa baina ya mtumaji na mpokeaji ili kuendelea kupunguza uwezo wa jumbe hizo kusambaa kwingineko na hivyo kudhibiti taarifa za uongo kusambaa

 

Mwishoni mwa mwaka uliopita, vyombo vya habari vya nchini India vililiripoti kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikizingatia mabadiliko Facebook na WhatsApp katika udhibiti wa maudhui ambapo mabadiliko hayo yametajwa kuwa ni changamoto katika matumizi ya teknolojia.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment