testiingg
The House of Favourite Newspapers

Taasisi ya Lalji Foundation Yaendesha Kambi ya Macho, 100 Wafanyiwa Upasuaji

0

Taasisi ya LALJI FOUNDATION inayojishughulisha na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii imefadhili kambi ya macho iliyofanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Geita Mkoani Geita ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake ya kuendelea kusaidia watu wenye matatizo ya macho.

Akizungumza wakati wa kambi hiyo Mwenyekiti wa taasisi ya LALJI FOUNDATION Ndugu Imtiaz Lalji amebainisha kuwa jumla ya watu 1578 walifanyiwa uchunguzi huku watu 100 wakifanikiwa kufanyiwa upasuaji baada ya kubainika kuwa na matatizo wakati wa uchunguzi.

Kuhusu muitikio wa watu katika kambi hiyo Mwenyekiti huyo amesema kuwa ni mkubwa na watu wengi wamejitokeza kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa macho.

Amesema taasisi hiyo itaendelea kuweka kambi ya macho mkoani Geita kwasababu muitikio na uhitaji wa watu ni mkubwa hivyo zoezi hilo litakua endelevu ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Leave A Reply