Tabibu Riziki: Mrembo Anayesumbua Kichwa Kugundua Dawa Ya Corona

 

Pengine umezoea kukutana na wataalamu wa tiba asilia, wanaume, tena wengi wakiwa na umri mkubwa! Habari zikufikie kwamba licha ya mwonekano wake, mwanamke mrembo anayekwenda na wakati, Tabibu Riziki Nkya ni moto wa kuotea mbali katika masuala ya tiba asili.

Tabibu Riziki, Mkurugenzi wa Kliniki ya JKBRS iliyopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ni tabibu aliyebobea kwenye matibabu ya tiba asili, akitumia mitishamba kukabiliana kirahisi na magonjwa mengi, yakiwemo yale yanayowasumbua watu wengi, ambayo tiba zake zimekuwa ngumu mahospitalini.

ALIINGIAJE KWENYE UTABIBU?

“Mimi ni mzaliwa wa Lyamungo Kati, Machame mkoani Kilimanjaro. Tangu nikiwa mdogo nimelelewa na bibi yangu Mahija Muro. Kwa sasa ni marehemu na alifariki dunia akiwa na karibu miaka 130, Mungu amlaze mahali pema peponi.

“Bibi yangu alikuwa tabibu, akiwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwa kutumia mitishamba. Tulikuwa tukiongozana naye kila alipokuwa akienda kutafuta dawa porini, huo ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuzijua dawa mbalimbali.

“Marehemu bibi yangu Mahija alipofariki aliniacha kwenye mikono ya bibi yangu mwingine, Mariam ambaye naye aliendelea kunifundisha mambo mbalimbali kuhusu tiba za asili na nilianza kuwasaidia watu tangu nikiwa mdogo, watu wengi wakawa wananiambia kwamba nitakuja kuwa daktari au tabibu mkubwa nikiwa mkweli, kwa hiyo hizi ni ndoto nilizotoka nazo utotoni,” anasema.

ALIVYOIANZA SAFARI YAKE

Tabibu Riziki anaendelea kueleza kwamba baada ya kupata elimu ya darasani, aliamua kukiendeleza kile alichokianza tangu akiwa mdogo.

“Niliwatafuta wataalamu mbalimbali wenye uelewa juu ya namna ya kuchakata madawa ya mitishamba bila kuharibu ubora wake, kwa sababu teknolojia hivi sasa imekuwa kubwa. Haikuwa kazi nyepesi lakini baada ya kuhangaika sana, nilifanikiwa kuanzisha Kampuni ya JKBRS ambayo makao makuu yake ni Ubungo Plaza, Ghorofa ya chini (Ground Floor) ambapo mimi ndiyo mkurugenzi wake.

“Lakini pia mimi na wenzangu tukafanikiwa kufungua kiwanda cha kutengeneza madawa ya mitishamba kwa teknolojia ya kisasa!

“Kwa hiyo kazi kubwa kwa sasa ni kwenda vijijini kukusanya dawa mbalimbali zinazotibu magonjwa mengi yanayowasumbua binadamu, kisha nikija naelekea kiwandani, nasimamia mwenyewe kuhakikisha zinatengenezwa kitaalamu ili ziweze kudumu kwa muda mrefu lakini pia ziwe na ubora wa hali ya juu.

DAWA ANAZOZIZALISHA

Tabibu Riziki anaendelea kueleza kwamba anazo dawa za aina mbalimbali anazozizalisha kwa kutumia mitishamba, zinazoendelea kufanya maajabu katika medani ya tiba za asili.

Miongoni mwa dawa hizo ni Life inayotajwa kuwa bora kutibu zaidi ya magonjwa zaidi ya 18, ikiwemo kisukari, kuimarisha kinga ya mwili, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, matatizo ya figo, maambukizi sugu katika njia ya mkojo (UTI) na mengine mengi.

“Dawa zetu nyingine ambazo zimeendelea kufanya maajabu kwa kutibu magonjwa ambayo hata hospitalini yameshindikana, ni Mushana inayopambana na Malaria sugu, DFP inayotibu meno yaliyotoboka na kuoza, fizi kutoa damu na kukaza meno yaliyolegea bila kukulazimu kuyang’oa.

“Lakini pia tunayo Joy inayotibu matatizo ya uzazi kwa wanawake, kama unavyojua tena suala la afya ya uzazi kwa wanawake huwa na changamoto nyingi, dawa yetu inao uwezo wa kuzimaliza karibu zote,” alisema Tabibu Riziki.

KUHUSU DAWA YA KUTIBU CORONA

Wakati dunia nzima ikiendelea na vita kali dhidi ya adui asiyeonekana kwa macho lakini mwenye madhara makubwa sana, Virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, Tabibu Riziki naye hayupo nyuma, anaendelea kuumiza kichwa na anasisitiza kwamba lazima tiba itapatikana.

“Tayari kuna dawa ambazo nimezigundua ambazo zinamsaidia mtu ambaye anashindwa kupumua. Hata kama hali ni mbaya kabisa, mtu hawezi kuvuta wala kutoa hewa, akitumia dawa hizi, kifua huwa kinaachia na kumfanya arudi kwenye hali ya kawaida.

“Haya ni mafanikio makubwa kwenye kupambana na Corona kwa sababu kama unavyojua kinachokatiza maisha ya watu wengi wenye maambukizi ya Corona, ni kushindwa kupumua kutokana na mapafu kujaa maji,” alisema Tabibu Riziki.

UPATIKANAJI WA DAWA ZAKE

“Dawa zetu zinapatikana karibu nchi nzima, tunao mawakala wanaotusaidia kuhakikisha zinapatikana kila mahali. Kwa mtu yeyote ambaye atakuwa anahitaji huduma zetu, anaweza kufika katika ofisi zetu zilizopo Ubungo Plaza, ‘ground floor’.

“Pia unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu 0744 111 115 au 0676 352 352,” anahitimisha.

Na Mwandishi Wetu


Loading...

Toa comment