The House of Favourite Newspapers

Binti Miaka 19 Ajifungua Watoto Watano Tabora – Video

BINTI mwenye umri wa miaka 19, Monica David, aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitano amejifungua watoto watano katika muda wa siku mbili.

Monica  alifikishwa hospitalini ambapo siku ya kwanza ambapo alijifungua mtoto mmoja na siku ya pili alijifungua watoto wanne.

Hata hivyo, watoto hao waliokuwa wa jinsia ya kiume wote hawakuweza kuishi kwa sababu walizaliwa kabla ya muda.

Akihojiwa, baba wa watoto hao ameelezea kusikitishwa na vifo vya watoto wake kwani siku zote maombi yake yalikuwa kupata mtoto wa kiume.

Hali ya afya ya binti huyo inaendelea vizuri.

Chanzo:CG FM Radio.

Comments are closed.