TACAIDS Waipongeza Kampuni ya Cool Blue
TUME ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) leo Novemba 6, 2019 imetembelea Kampuni ya maji safi ya Cool Blue Mikocheni jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kuwafanya watu wajiepushe na kuwa waangalifu kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi na kuiona kampuni hiyo ni moja katika mapambano ya kudhibiti Ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mtedaji wa TACAIDS, Dkt. Leonrad Maboko, alisema kuwa ameuona mchango wao wa muda mrefu sana kupitia karatasi lililo kwenye maji hayo, ambao ni muhimu sana kuwakumbusha watu kuhusiana na Ugonjwa huo na ndio maana waliwatembea kwaajili ya kuwapa motisha zaidi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya maji safi ya Cool Blue, Fauzia Malik ameipongeza TACAIDS kwa kutambua mchango wao wa kutoa elimu ya Ukimwi kupitia maji yao ya Cool Blue na wataendelea kuelimisha jamii.
HABARI NA IMELDA MTEMA | GPL
Comments are closed.