The House of Favourite Newspapers

TADB Yashiriki Maonesho Ya Wiki Ya Maziwa Mkoani Tabora

0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde (kushoto) akipata kutoka kwa Joseph Mabula Mratibu wa Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) unaoratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya wiki ya maziwa yanayofanyika mkoani Tabora. TADB kwa kushirikiana na wadau wengine wanatekeleza mradi wa T13P unaolenga kuwanufaisha wafugaji wadogo 100,000 wa ng’ombe wa maziwa pamoja na wachakataji. 
Afisa Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Patrick Kapungu (wa pili kulia) akizungumza na mteja aliyetembelea banda la TADB katika maonesho ya wiki ya maziwa yanayofanyika kitaifa mkoani Tabora. TADB kwa kushiriana na wadau mbalimbali inatekeleza Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) utakaowanufaisha wafugaji wadogo 100,000 wa ng’ombe wa maziwa pamoja na wachakataji maziwa.                                                          
Mratibu wa Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) Joseph Mabula (kulia)akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi huo ambao walishiriki katika maonesho ya wiki ya maziwa inayiofanyika mkoani Tabora.                                                                                                                
Kaimu meneja wa kanda ya Mgharibi Benki ya Maendeleo Tanzania (TADB) Furaha Sichula (kulia) akiteta jambo na Mark Tsoxo Mkuu wa Programu wa shirika la Heifer International wakati wa maonesho ya wiki ya maziwa yanayofanyika mkoani Tabora. TADB, Heifer International na Land’O Lakes wanashirikiana kutekeleza a Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) unaolenga kunufaishawafugaji wadogo 100,000 wa ng’ombe wa maziwa pamoja na wachakataji wa maziwa.
Leave A Reply