The House of Favourite Newspapers

TAHARUKI, MWILI ULIOZIKWA JULAI WAFUKULIWA SEPTEMBA

0
maiti yafukuliwa
Zoezi la kufukua likiendelea.

 

KILIMANJARO: Taharuki! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kufuatia umati mkubwa wa watu kujitokeza jana wakati polisi walipoongoza ufukuaji wa kaburi la marehemu Juma Hamis kwa amri ya Mahakama huko Pasua, mjini Moshi.

 

Chanzo cha kuaminika kililieleza Risasi Mchanganyiko, kuwa marehemu alifariki dunia baada ya kupigwa na wananchi Aprili mwaka huu kwa kudaiwa kubaka mke wa mtu. Inadaiwa baada ya mume wa mwanamke aliyebakwa kupata taarifa hizo, alimtafuta marehemu ambaye ni mwendesha bodaboda na kumnasa kisha kumpigia yowe la ubakaji, ndipo alipozingirwa na wananchi na kupata kipigo kikali.

maiti yafukuliwa
Gari la Polisi eneo la tukio.

 

“Yule bodaboda alipigwa mno na wananchi kiasi kwamba akawa hoi na hajitambui. Baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya KCMC ambako alilazwa kwa
kipindi cha miezi mitatu mpaka mauti yalipomkuta Julai 28 mwaka huu,” kilisema chanzo hicho.

 

Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa, hata hivyo baada ya kutokea tukio hilo la kupigwa kwa bodaboda huyo, hata kabla ya kifo chake, taarifa zilianza kuenea kwamba kumbe siyea aliyetenda tukio hilo.

 

“inavyoonekana yule mwenye mke hakupewa taarifa vizuri juu ya mtu aliyembaka mkewe. Kwa hiyo akajikuta anamsababishia kifo mtu mwingine kabisa ambaye hakuhusika.

 

“Sasa wale ndugu wa huyo mtu hawakukubali. Waliamua kwenda kutoa taarifa k w e n y e v y o m b o vya sheria, yule ambaye mkewe anasadikika kubakwa a k a t i w a m b a r o n i a m b a p o mpaka sasa anashikiliwa na polisi. “Hicho ndicho kilichotokea, lakini kilichovuta zaidi hisia za watu wengi ni kwamba wakati mwili wa marehemu unafukuliwa umekutwa upo vizuri, utafikiri marehemu alikufa jana. “Haujaharibika kabisa, wala hautoi harufu yoyote,” kilisema chanzo hicho.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Selemani Issa alipotafutwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kwamba lilifanywa na serikali ili kusaidia katika upelelezi. “Kwani ni jambo la ajabu kaburi kufukuliwa? Hiyo ni kawaida katika kukamilisha upelelezi, huyo mtu aliuawa, sasa ni lazima tujiridhishe na kilichosababisha kifo chake ili taratibu nyingine ziendelee,” alisema kamanda huyo.

maiti yafukuliwa
RPC Kilimanjaro.

 

Uthibitisho wa kutokea kwa jambo hilo lililovuta umati mkubwa wa watu, ulitolewa pia na Mtendaji wa Kata ya Pasua, Josephat Mmbonyo.

 

“Hata hivyo ni ukweli kwamba kufukuliwa kwa kijana huyo kumezua taharuki maana kwa muda aliofariki na kuzikwa, ilikuwa si rahisi kukuta mwili wake ukiwa haujaharibika,” alisema mtendaji huyo.

 

STORI: BONIPHACE NGUMIJE NA GABRIEL NG’OSHA| RISASI

Leave A Reply