TAHIYA AMSUSIA BWANA MOBETO

Tahiya John

VIDEO Queen Tahiya John ambaye hivi karibuni alifunguka kuchukuliwa bwana na mwanamitindo Hamisa Mobeto ameonekana kumsusia bwana huyo baada ya Hamisa kuonekana akiwa ameongozana naye kwenye Tuzo za SZIFF wiki iliyopita.  

 

Gazeti la Risasi Jumamosi baada ya kumuona Hamisa akiwa ameongozana na bwana huyo liliamua kumsaka Tahiya ili kufahamu kama ameachana na bwana huyo mazima na kumuachia Mobeto ambapo alifunguka kama ifuatavyo:

Risasi Jumamosi: Tahiya vipi umeachana na mpenzi wako? Mbona juzikati alionekana na Mobeto kwenye Tuzo za SZIFF.

Tahiya: Du, nakufa mimi…

Risasi Jumamosi: Unakufa nini si utuambie je, umeachana naye?

Tahiya: Siwezi kusema nimeachana naye au sijaachana naye.

Risasi Jumamosi: Sasa mbona wameonekana SZIFF wameongozana na wewe upo?

Tahiya: Bwana ee kama wameo-ngozana watajijua wenyewe mimi sitaki kuwazu-ngumzia kabisa.

 

TUMEFIKAJE HAPA

Tahiya na bwana huyo anayedaiwa kuwa mpenzi mpya wa Mobeto walikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa kuishi pamoja kupika na kupakua ambapo hivi karibuni mrembo huyo alidai kumfumania Mobeto hotelini huko Zanzibar kitendo kilichozua gumzo kubwa mitandaoni. Hata hivyo, baada ya siku kadhaa wadau wa mitandaoni waliibuka na kumnanga Mobeto wakidai kuwa bwana huyo amerejea kwa mpenzi wake (Tahiya).

Juzikati bwana huyo alionekana akiwa ameongozana na Hamisa kwenye Tuzo ndipo watu mitandaoni wakaibuka tena na kuanika kuwa wapenzi hao hawakuachana baada ya kufumaniwa na sasa mambo yapo hadharani. Hamisa aliposakwa kumzungumzia mpenzi wake huyo mpya alipokea simu na baada ya kuelezwa madai hayo alikata bila kusema chochote

STORI: Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Toa comment