Tahiya: Hamisa hawezi kuwa mke mwenzangu

MREMBO wa mjini, Tahiya John amemvaa kwa mara nyingine mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto na kusema kuwa hawezi kuwa mke mwenzake.

Wikiendi iliyopita, Tahiya alitupia picha yake kwenye mtandao ambapo mtu mmoja alimuita mke mwenza wa Hamisa, ndipo akamjibu; “Hawezi kuwa mke mwenzangu.”

Gazeti hili lilimuuliza Hamisa kuhusiana na ujumbe huo wa Tahiya ambapo alisema hana muda mchafu wa kujadili mambo ya mtandaoni.

 

 STORI: IMELDA MTEMA, DAR


Loading...

Toa comment