Kartra

Taifa Stars Vs Libya..Mechi Ya Heshima, Kisasi Leo

   NI mechi ya heshima na kisasi kwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambapo leo Jumapili itakapoikaribisha Libya kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mechi hiyo ya kufuzu AFCON 2022, haina faida kwa yeyote kati ya timu hizo zaidi ya kulinda heshima na kulipiza kisasi kutokana na timu hizo zilizopo Kundi J, zote kutokuwa na nafasi ya kufuzu michuano hiyo na leo ndiyo mechi ya mwisho.

Taifa Stars inataka kulipiza kisasi cha kufungwa 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa kule Libya, lakini pia itataka kumaliza hatua hiyo kwa heshima, hivyo ushindi kwao ni muhimu.Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, huu utakuwa ni mchezo wake wa pili wa kimashindano tangu akabidhiwe kikosi hicho ambapo mechi ya kwanza alipoteza kwa Equatorial Guinea 1-0.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema: “Timu imefanya mazoezi ya mwisho leo (jana Jumamosi) kuelekea mchezo wa kesho (leo Jumapili).“Hakuna majeruhi, wachezaji wana morali ya kupambana ili kupata pointi tatu kwenye mchezo huo.

 

”SAFU YA ULINZITimu zote zikiwa zimecheza michezo mitano, Taifa Stars ni imara kwenye upande wa ulinzi ambapo imeruhusu mabao sita, huku Libya ikiruhusu 14.

SAFU YA USHAMBULIAJITaifa Stars haipo vizuri kwenye ushambuliaji kwani ina mabao manne, huku Libya ikifunga saba.


Toa comment