Taifa Stars yaendelea na mazoezi Afrika Kusini
Kutoka kushoto, Ibrahim Ajib , Jonas Mkude na Said Ndemla (nyuma yao) wakiwa katika mazoezi ya kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars leo kwenye Uwanja wa Edenvale kwenye kitongoji cha Edenvale jijini Johannesburg, Afrika Kusini..
Beki wa kati wa Stars, Hassan Isihaka (kulia) akijiandaa kumpiga chenga kiungo wa timu hiyo, Mudathir Yahaya.Kocha wa makipa wa Stars, Manyika Peter (kushoto) akiwanoa makipa wake leo jijini Johannesburg.
Beki wa kati wa Stars, Hassan Isihaka akiwania mpira mbele ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva huku Salum Aboubakary ‘Sure Boy’.
Kiungo wa Stars, Frank Domayo (kushoto) katika harakati za kuwania mpira na kiraka, Salum Telela kwenye mazoezi ya Stars inayojiandaa na mchezo dhidi ya Algeria wa kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia, 2018 utakaopigwa Novemba 14, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Kikosi cha Taifa Stars kikiendeleza tizi, k.utoka kushoto ni kipa Aishi Manula, Nadir Haroub ‘Cannavaro (nahodha), Juma Abdul na Farid Musa.Beki wa kulia wa Stars, Hassan Kessy (kulia) akimili mpira mbele ya kiungo Frank Domayo katika mazoezi ya kikosi hicho nchini Afrika Kusini. Simon Msuva (wa kwanza kushoto) akiwa tayari kutoa msaada.Kipa wa Stars, Ally Mustafa akifanya mazoezi ya kuruka koni leo asubuhi akijiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Algeria.
(PICHA NA SALEH ALLY/ GPL, JOHANNESBURG)