Taifa Stars Yagawana Pointi na DR Congo

TIMU ya Taifa ya Kandanda ya Tanzania, Taifa Stars ikiwa ugenini imefanikiwa kugawana pointi na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC  baada ya kupata sare ya 1-1, kwenye mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022.

 

Mchezo huo umepigwa leo Septemba 2, kwenye uwanja wa klabu T.P Mazembe katika mji wa  Lubumbashi, DR Congo walikuwa wakwanza kutikisa nyavu za Taifa Stars kupitia kwa Mbokani Dieudonné dakika ya 23’ ya mchezo.

 

Baada ya goli hilo Stars walicharuka na kufanikiwa kusawazishwa kupitia kwa  nyota wa Wydad, Casablanca Simon Msuva dakika ya 36.

Kwa matokeo hayo Taifa  stars ina alama moja sawa ana DR Congo huku Benin na Madagascar wakipepetana usiku huu kwenye mchezo wa kundi J.

 


Toa comment