The House of Favourite Newspapers

Taiya Alazimishwa Kupima

MUIGIZAJI anayekuja kwa kasi kwenye anga la uigizaji, ambaye anatamba kwenye Tamthiliya ya Kapuni inayorushwa na Kituo cha Televisheni ya Magic Swahili, Taiya Odero anadaiwa kulazimishwa na ndugu zake kwenda hospitali kupima afya yake baada ya kupukutika mwili.

 

Akizungumza na gazeti hili, mtu wa karibu na msanii huyo, alisema kuwa familia ya msanii huyo iliingilia kati afya yake na kumuambia kuwa ni lazima watampeleka hospitali licha ya mwenyewe kuwaambia kuwa hana tatizo lolote.

 

“Familia yake sasa hivi kama imepoteza amani kwa sababu ya ndugu yao. Wanataka kumpeleka hospitali kucheki afya yake wakati yeye anasema yuko sawa hakuna kinachomsumbua kabisa,” kilisema chanzo.

Kwa upande wake, Taiya alipotafutwa na Amani, alisema kuwa kama familia lazima iingiwe na hofu lakini yeye yuko sawa na hana tatizo lolote la kiafya bali alikuwa amepunguza kula vyakula vya kumnenepesha.

“Sina tatizo lakini kama ndugu lazima waingiwe na hofu na mimi niko kwenye kuwaelewesha kuwa sina tatizo lolote,” alisema Taiya.

Stori: Imelda Mtema | Gazeti la Amani.

Comments are closed.