The House of Favourite Newspapers

TAKUKURU Kagera watoa onyo kwa wagombea uchaguzi serikali za mitaa

0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU mkoa wa Kagera imewataka wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotalajia kufanyaika Novemba 27 mwaka huu kutokujihusisha na vitendo vya rushwa kwani wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Ezekia Senkara wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa mkoa wa Kagera kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2024.

Aidha amebainisha kuwa wanaendelea na kazi ya uelimishaji wananchi kuelekea uchaguzi na mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kwa kosa la kutoa au kupokea rushwa wala shahuri lililofikishwa mahakamani.

Leave A Reply