The House of Favourite Newspapers

Takukuru wamtaja tajiri anayeingiza Sh. Mil 7 kila dakika

0

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi Said

By Julius Mathias

SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kueleza juu ya hujuma ya uchumi inayofanywa na mtu anayeingiza Sh7 milioni kila dakika, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemtaja Mohammed Mustapha Yusufali kuwa nyuma ya tuhuma hizo.

Juzi, Rais Magufuli alieleza kuwa kuna mtu ambaye ana kampuni inayotoa Mashine za Kielektroniki za Hesabu za Fedha (EFD), nje ya mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzisambaza kwa wafanyabiashara na kutokana na mtandao wake hujiingizia Sh7 milioni kila dakika.

Alieleza kuwa mtandao wake unashirikisha watumishi wa TRA na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) na kuisababishia Serikali yake hasara ya mabilioni.

Jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola akiwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwapo kwa kampuni nne ambazo zimekwepa kodi ya Sh30 bilioni na kuzipa   hadi Julai 5, ziwe zimelipa fedha hizo kabla hajazifikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Chanzo: Mwananchi

Leave A Reply