The House of Favourite Newspapers

Talib Aungana na Simba Kusaidia Jamii Atoa Misaada kwa Vituo Vitatu

0

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Oman ya Beach Soccer, Talib Hilal, ambaye pia aliwahi kuichezea Simba, ameungana na Simba, katika kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea Watoto Yatima vya jijini Dar es Salaam, ikiwa kama moja ya kampeni ya kuelekea kilele cha Simba Day, katika kurejesha kwa Jamii.

 

Talib ameungana na uongozi wa Simba ambao wiki hii wanarejesha fadhila kwa jamii kuelekea kilele cha tukio kubwa la kihistoria la Simba Day linalotarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Tukio hilo kubwa la kukabidhi vyakula llimefanyika mapema leo kwenye Ofisi za Global Group, zilizopo Sinza Mori, Dar, kwa kushirikiana na Kocha Talib.

Akizungumza na Waandishi Habari, Talib alisema kuwa kwa miaka minne amekuwa akitoa misaada kwa vituo hivyo vitatu ambavyo ni Mwana Orphans Centre cha Vingunguti, Tanzania kwanza Orphanage cha Tuangoma, Temeke na Mwandaliwa Orphanage cha Mbweni.

 

Talib alisema ataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na vitu kuwafikia wahitaji kwa wakati, huku akiwataka watu wengine kujitokeza kuwasaidia Watoto Yatima.

 

“Nimekuwa nikitoa misaada katika vituo hivi kwa kipindi cha miaka minne, na mara zote nimekuwa nikimtumia mwakilishi wangu kuwapatia kutokana na mimi kubanwa na majukumu.

“Hivyo ninajisikia furaha leo kukutana na walezi wa watoto hawa ambao nimepiga nao picha na kukaa nao pamoja.

“Nitoe wito kwa watu wengine kuwasaidia watoto hawa, kwani wasipopata malezi mazuri watapotea, nimetoa msaada huu katika kuunga mkono uongozi wa Simba ambao wiki hii wanatoa kwa jamii katika kunogesha tamasha la Simba Day,” alisema Talib.

 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kituo cha Tanzania Kwanza Orphanage, Hidaya Shomvi alisema kuwa “Kwa niaba ya wenzangu natoa shukrani kwa mlezi wetu Talib ambaye amekuwa akitupa misaada mara kwa mara.

 

“Watoto Yatima wanahitaji kupatiwa malezi mazuri, hivyo zipo changamoto nyingi tunazokabiliana nazo ambazo kwa kupitia misaada hii tunayoipata, inatusaidia sisi walezi kutatua ,abo kadha wa kadha,” alisema Hidaya.
mwisho

Leave A Reply