The House of Favourite Newspapers

Tamasha kubwa la instagram kufanyika Escape One keshokutwa

0

Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred NgimbaMkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kukusanya umati mkubwa wa watumiaji wa mitandao ya kijamii na wapenzi wa burudani.

IMG_6446Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Krantz Mwantepe (kulia) akimsikiliza kwa umakini mkurugenzi wake wakati akizungumza.
IMG_6436Hawa ni baadhi ya mapaparazi waliokuwa wakichukua taarifa hiyo.

WAPENZI wa burudani na watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram keshokutwa Jumamosi wanatarajiwa kufurika kwenye tamasha kubwa la burudani kwenye Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Freconic Ideaz, Fred Ngimba, waandaaji wa tamasha hilo, alisema katika tamasha hilo kutakuwa na wasanii lukuki watakaotoa burudani ingawa alisema watakuwa ‘surprise’ akimaanisha watatokea kwa kushitukiza.

Licha ya wasanii wa muziki, tamasha hilo litapambwa na wasanii wa luninga ambao wanatarajiwa kufurika kwenye ufukwe huo.

Ngimba alisema mashabiki watakaohudhuria tamasha hilo watapata fursa ya kupiga picha na kujiachia na wasanii hao watakavyo kuanzia mishale ya saa tatu za usiku mpaka majogoo.

(PICHA: RICHARD BUKOS / GPL)

Leave A Reply