The House of Favourite Newspapers

Tamasha la magari nchini kuja kivingine

0

Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko, Michael Kanyatta, Meneja Huduma wa kampuni ya Sanwa Service Ltd, Masao Kuwabara, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments, Ally Nchahaga, Meneja Masoko, Mori Bencus na Meneja kitengo cha huduma wa Vision, Dorah Raymond.

Meneja Huduma wa Kampuni ya Sanwa Service Ltd, Masao Kuwabara akizungumza jambo.

Mkutano ukiendelea.

Wanahabari wakichukua tukio.

TAMSHA la Magari nchini (Autofest) limerudi kivingine ikiwa ni mwaka wa nne sasa tangu kuanzishwa kwake.Tamasha hilo linakuja na mtoko mpya wa magari na pikipiki ambazo zitaoneshwa kwa matoleo mapya ikiwa ni moja ya maonyesho muhimu yenye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vision Investments, Ally Nchahaga ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo, amesema kuwa lengo ni kundeleza kuwapatia wadau wao aina mbalimbali za bidhaa za vyombo vya moto (Autofest) ili waweze kuridhishwa navyo.

Amesema kuwa katika tamasha hilo pia kutakuwa na uoshwaji wa magari kupitia watu maarufu wa hapa Tanzania ambapo fedha ya uoshaji huo itakayopatikana itatumika kwa ajili ya kusaidia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha wahanga wa ajali kupata kifaa “dedside Ultrasound ” pamoja na kuchangia hazina ya damu.

Aidha alifafanua kuwa tamasha hilo kubwa litaonyesha magari ya abiria, biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Septemba 18-19 mwaka huu kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar, huku burudani za kwenye tukio zitahusisha ‘Auto Style Zone’ ambayo itakuwa nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao na ‘Kids Car Zone’ambayo yatawaburudisha watoto.Kauli mbiu ya tamasha hilo ni “Defensive driving is key to road safety” huku mgeni rasmi wa tamsha hilo akitarajiwa kuwa, Katibu Mkuu wa viwanda na biashara.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

 

Leave A Reply