Tamasha la Marahaba Swahili Music Festival lilivyofana
Kikundi cha bendi kiitwacho, Afrijam band’ kutoka Bagamoyo – Pwani kikitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Bendi ya ‘Muswanu Gogo Vibes’ kutoka Sinza Dar wakitoa burudani.
Mwimbaji wa bendi ya nyimbo za asili, Isack Abeneko (kulia) akitawala jukwaa.
Mshiriki wa BSS 2015, Kevin Gerson akionesha ujuzi wake wa kuimba nyimbo (Live) kwenye hafla hiyo.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vikiendelea kutoa burudani.
Ni mzuka kwa kwenda mbele.
Msanii wa muziki kutoka nchini Burundi, Natacha Ngendabanka akionesha ujuzi wake kwenye hafla hiyo.
Msanii Natacha (kushoto) na mwenzake kutoka nchini Burundi wakiendelea kuonesha ujuzi wao.
Natacha akiimba huku ameshikilia bendera ya nchini kwao.
Msanii wa muziki kutokea nchini Uganda, Muserebende Hytham ‘Ssali’ naye akionesha manjonjo yake.Mashabiki wakifuatilia burudani za nyimbo za asili zilizokuwa zikiimbwa live.Mashabiki wakiendelea kupata burudani vya kutosha.
HIVI ndivyo hali ilivyokuwa kwenye tamasha la muziki wa asili lililopewa jina ’Marahaba Swahili Music Festival’ jana na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dar waliopata burudani mbalimbali za muziki wa ngoma za asili na nyimbo mbalimbali zilizoimbwa (Live).
Akichonga na mtandao huu, mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Fatma Saleh amesema kuwa tamsha hilo ni la tatu kufanyika hapa nchini na lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii chipukizi wanaoimba na kupiga ngoma za asili.
Amesema tamasha hilo pia hutumika kama ishara mojawapo ya kuendeleza utamaduni wetu kwani hukutanisha wasanii mbalimbali.
Fatma aliongeza kuwa mbali na wasanii wa hapa nchini pia wapo wasanii kutoka nchini Burundi,Natacha na bendi yake pamoja na msanii wa Uganda, Muserebende ytham’Ssali’ ambao nao walifika kwa ajili ya kuwapa sapoti ya kuimba nyimbo mbalimbali za nchini kwao.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
Comments are closed.