Tamasha La Watu wa Iran Lilivyonoga Sabasaba, Mkurugenzi Tantrade Atia Neno
Dar es Salaam 8 Julai 2024: Siku ya Tamasha ya Iran ilivyonoga katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ambapo wafanyabiashara watanufaika na Muungano ya nchi zote mbili.
Akizungumza Leo Julai, 8, 2024,kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar, Mkurugenzi wa Tantrade, Bi. Latifa Khamis amesema leo imekuwa ni siku nzuri sana kwa sababu nchi hizi mbili, zimeonyeaha Ushirikiano mkubwa wa kibiashara,na kupelekea wafanyabiashara kunufaika kwa kuwa bishaa ambazo zinatoka Tanzania zinapelekwa Iran na za Iran zinaletwa Tanzania hivyo kuleta tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi hizi mbili.
“Tumejifunza mengi sana kwa wenzetu hawa wa Iran ambao kiukweli wako vizuri sana kwenye mambo mbalimbali kama vile tulivyojionea upande wa madawa yao ya kupambana na sumu za viumbe hatari kama vile nyoka, nge na viumbe wengine hatari”. Alisema Bi.Latifa
Katika tamasha hilo watu wa Iran walionesha vitu vyao mbalimbali vya kitamaduni ikiwemo madawa, vyombo vya nyumbani na mengineyo.