MIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, inatarajia kukutana leo Jumatano katika Uwanja wa Taifa, Da es Salaam kuondoa ubishi unaoendelea kwa sasa.
Mchezo huu ni wa Ngao ya Jamii ambao u n a a s h i r i a kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu, i n a y o t a r a jiwa kuanza k u t i m u a vumbi Agosti 26 kwa timu 16 k u s h u k a dimbani.
Championi Jum a t a n o l i n a k u letea tambo mbalimbali za wachezaji na m a kocha kuelek e a m c h ezo huo u t a k a oanza kup i g w a saa 10:00 jioni leo.
SHIZA KICHUYA
“Tumejiandaa vizuri na mchezo huo kwa kuwa kikosi chetu kipo vizuri na tunahitaji kushinda.
“Kwa upande wa wachezaji hatuna mchezaji atakayetusumbua katika mchezo huo zaidi ya Ibrahim Ajibu ambaye kiwango chake tunakifahamu vizuri hakuna asiyekijua.”
HARUNA NIYONZIMA
“Siku zote mechi ya Simba na Yanga ni kubwa na ni ngumu, na si kwa sababu nipo huku ndiyo niseme hivyo, hata nilivyokuwa Yanga mechi hii tulikuwa tukiichukulia kwa umakini wa hali ya juu.
“Tunahitaji kujipanga ili tuweze kushinda mchezo huu, nimejiandaa vizuri ili niweze kuisaidia timu yangu iweze kushinda.”
NADIR HAROUB ‘CANNAVARO’
“Derby ya Simba na Yanga itakuwa nzuri na siku zote mchezo huu hauwezi kuutabiri, yeyote atakayefanya vizuri atashinda, tusubiri dakika 90.”
ABDALLAH SHAIBU ‘NINJA’
“Watu wanaoongea vibaya kuhusu mimi, basi wasubiri timu yao tutakapokutana Taifa, wasubiri kuona muziki wangu.”
GADIEL MICHAEL
“Sina wasiwasi wowote na Simba kuelekea katika mchezo huu, kutokana na maandalizi makubwa tuliyoyafanya.
“Tupo katika maandalizi makubwa sana, naamini Simba hawana pa kutokea, timu yetu ipo vizuri kupambana na timu yoyote kwa sasa na si Simba pekee.”
EMMANUEL OKWI
“Naamini wapinzani tukikutana nao tutawafunga mapema tu kutokana na kikosi chetu kukamilika kila idara, kwa maana kwamba kila mmoja wetu anatimiza majukumu yake ipasavyo.”
GEORGE LWANDAMINA
“Huku sisi tupo vizuri, tunaendelea na mazoezi kama kawaida, kikubwa ambacho naweza kusema ni kwamba vijana wangu kila siku wanazidi kuwa imara na kunipa matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Simba.
“Kwa namna siku zinavyozidi kwenda, naona tupo tayari kwa mchezo huo, wapinzani wetu waje tu tupambane.”
JOSEPH OMOG
“Kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya kucheza na Yanga kwa sababu kila ambacho nilipanga kukitoa kwa wachezaji kimekamilika na wamekishika kwa jinsi ambavyo nataka.
“Nikwambie tu kuwa hatuna presha na wapinzani wetu kwa sababu natambua tumeshacheza nao na tumepata matokeo mazuri mbele yao, imani yangu ni kwamba lazima tutapata matokeo mazuri mbele ya wenzetu hao.”
Simba vs Yanga, Uwanja wa Taifa Hapatoshi, Sikiliza Tambo za Mashabiki
Stori: Khadija Mngwai | Championi Jumatano