The House of Favourite Newspapers

Tambwe Aitangazia Vita Simba

0

Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI JUMNATATU| Dar es Salaam

BAADA ya juzi Jumamosi, mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe kuiongoza timu yake hiyo kutinga nusu fainali ya Kombe la FA, amesema kuwa makali yake hayo anayahamishia ligi kuu.

 Katika mechi hiyo ya Kombe la FA ambayo Yanga ilicheza dhidi ya Prisons na kushinda mabao 3-0, bao moja kati ya hayo lilifungwa na Tambwe.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema kuwa anataka kuona Yanga ikishinda mechi zake zote zilizobakia na kuiondoa Simba katika nafasi ya kwanza ambayo inashika hivi sasa.

“Namshukuru Mungu nimeanza vizuri baada ya kupona majeraha ya goti yaliyokuwa yakinisumbua na sasa nguvu zangu zote nazielekeza katika mechi zetu za ligi kuu zilizobakia.

“Tumebakiza mechi tano, endapo tutashinda zote hizo tena kwa idadi nzuri ya mabao, tutakuwa tumewapoteza Simba na sisi kuwa mabingwa kwa mara nyingine tena,” alisema Tambwe ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu mara mbili tena kwa idadi kubwa ya mabao.

Mara ya kwanza kutwaa tuzo hiyo ilikuwa msimu wa 2013/14 ambapo alifunga mabao 19 na mara ya pili ilikuwa msimu uliopita wa 2015/16 ambao alifunga mabao 21.

Mwanariadha Mtanzania Simbu Avunja Rekodi Nyingine England Marathons

Leave A Reply