Tambwe ampora Okwi tuzo, ampa Makambo

Heritier Makambo

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Heritier Makambo, ametabiriwa kuwa ndiye atakayekuwa mfungaji bora msimu huu tena kwa kuzivunja rekodi mbili zilizowekwa na wachezaji wenzake wa kimataifa wanaocheza soka hapa nchini.

 

Rekodi hizo ambazo Makambo ametabiriwa kuzivunja ni ile ya mshambuliaji mwenzake wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe aliyoiweka msimu wa 2015/16 baada ya kufunga mabao 21 lakini pia ile ya msimu uliopita wa 2017/18 iliyowekwa na mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi ambaye alifunga mabao 20.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja alisema kuwa Makambo ndiye atakayekuwa mfungaji bora msimu huu na siyo Okwi kutokana na ubora wake wa kuzifumania nyavu ambao ameuonyesha katika mzunguko wa kwanza na anaweza kuzivunja rekodi hizo mbili. Alisema mpaka sasa wakati Yanga imebakiza mechi moja kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, Makambo amefunga

Loading...

Toa comment